Legal:Generic screener survey privacy statement for design research/sw
Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Generic screener survey for design research. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.
Kukusanya na Kutumia Maelezo
Sababu ya kukusanya maelezo yako
Mradi huu utatusaidia kuboresha mazingira ya mtumiaji. Tutatumia maelezo unayotupa:
- Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
- Kupata wanaotuma maombi, washiriki au teuzi
- Kukuza maarifa kupitia utafiti wa wazi
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali tuma barua pepe kwa desresadmin wikimedia.org.
Jinsi tunavyokusanya maelezo yako
Google Forms hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake. Qualtrics hutumiwa pia kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.
Maelezo tunayokusanya
Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.
- Majibu ya maswali
- kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
- Maelezo ya demografia
- kama vile utaifa, jinsia
Kushiriki
Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako
Hakuna kuchapisha: Maelezo tunayokusanya hayatashirikiwa hadharani.
Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.
Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.
Ulinzi
Muda ambao tunahifadhi maelezo yako
Data tunayokusanya itafutwa, kutolewa utambulisho, au kujumlishwa ndani ya siku 90. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.
Mtu wa kuwasiliana naye
Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa desresadmin wikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.