Legal:Event Registration Tool Feedback Privacy Statement/sw
Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Event Registration Tool Feedback. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.
Event Registration Tool Feedback | |
---|---|
Kutoka Campaigns team | |
Data tunayokusanya itatumika kukagua au kuimarisha huduma zetu | |
Data Iliyokusanywa | |
Majibu | Ndiyo |
Maelezo ya mawasiliano | Ndiyo |
Data ya demografia | Ndiyo |
Kurekodi | Hapana |
Data iliyochapishwa | |
Yasiyotambulisha | Ndiyo |
Yanayotambulisha | Hapana |
Ufikiaji wa Data | |
Wikimedia Foundation | Ndiyo |
Wanaojitolea | Hapana |
Mshiriki | Yux |
Watoa huduma |
|
Hifadhi ya Data na Ufutaji | |
Uzuiaji wa Data Ghafi | Siku 90 |
Eneo la Data | Marekani na maeneo mengine |
Tafadhali soma Taarifa kamili ya Faragha |
Kukusanya na Kutumia Maelezo
Sababu ya kukusanya maelezo yako
Mradi huu utatusaidia kutambua mada zenye tija, kuboresha mazingira ya mtumiaji. Tutatumia maelezo unayotupa:
- Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
- Kuwasiliana nawe zaidi
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali soma ukurasa wake husika.
Jinsi tunavyokusanya maelezo yako
LimeSurvey hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.
Maelezo tunayokusanya
Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.
- Majibu ya maswali
- kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
- Maelezo ya mawasiliano
- kama vile jina, jina la mtumiaji, anwani ya barua pepe
- Maelezo ya demografia
- kama vile utaifa, jinsia
Kushiriki
Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako
Kuchapisha: Tutachapisha tu data isiyotambua (kama vile manukuu, takwimu zisizo na majina au data nyingine ya jumla). Ili kuwezesha uchapishaji huu, unakubali kuchangia michango yako yenye hakibunifu kwa kikoa cha umma chini ya masharti ya Creative Commons Zero 1.0.
Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua. Tafadhali fahamu kwamba tunashirikiana na Yux, ambaye pia anabanwa na majukumu ya mkataba kuzingatia maelezo yako mara kwa mara kwa kanuni za Sera yetu ya Faragha.
Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.
Ulinzi
Muda ambao tunahifadhi maelezo yako
Data tunayokusanya itafutwa, kutolewa utambulisho, au kujumlishwa ndani ya siku 90. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.
Mtu wa kuwasiliana naye
Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa campaign-tools wikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.