Legal:Event Registration: Organizer Experiences Video Privacy Statement/sw
Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Event Registration: Organizer Experiences Video. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.
Kukusanya na Kutumia Maelezo
Sababu ya kukusanya maelezo yako
Mradi huu utatusaidia tathimini, thibitisha na zoea, kuwekeza katikamaendeleo ya ujuzi na uongozi na kuboresha mazingira ya mtumiaji. Tutatumia maelezo unayotupa:
- Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
- Kuwasiliana nawe zaidi
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali soma ukurasa wake husika.
Jinsi tunavyokusanya maelezo yako
Google Forms hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake. Google Meet hutumiwa pia kuandaa mkutano au kutiririsha tukio; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.
Maelezo tunayokusanya
Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.
- Majibu ya maswali
- kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
- Maelezo ya mawasiliano
- kama vile jina, jina la mtumiaji, anwani ya barua pepe
- Rekodi
- kama vile video, sauti, picha
- Hati
- kama vile rekodi za gumzo, manukuu, picha za skrini
Kushiriki
Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako
Kuchapisha: Tutachapisha data ya kutambua (kama vile manukuu ya moja kwa moja pamoja na sifa). Ili kuwezesha uchapishaji huu, unakubali kuchangia michango yako yenye hakibunifu kwa kikoa cha umma chini ya masharti ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 na 4.0.
Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.
Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.
Ulinzi
Muda ambao tunahifadhi maelezo yako
Data ghafi tunayokusanya inaweza kuhifadhiwa kwa muda usiobainika. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.
Mtu wa kuwasiliana naye
Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa ifried wikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.